Friday, 2 June 2017

Trump alizuiwa kutumia simu hii baada ya kuapishwa

 Mwandishi wa habari za kisiasa na mhariri wa AXIOS Media, Mike Allen, anasema Rais Trump anatumia simu ya iPhone na kwamba simu yake imewekwa App ya Twitter tu.

Sababu ya kufanya hivyo na kumuwekea App hiyo ni kupunguza hatari ya uwezekano wa simu yake kudukuliwa. Aidha pia kumpunguzia muda wa matumizi ya simu na ili ajielekeze zaidi katika mambo ya kiofisi zaidi.

Simu ya awali ambayo alizuiwa kuitumia baada ya kuwa Rais ilikuwa ni Samsung. Alibadili kutoka Android kwenda iOS mwezi Machi mwaka huu.

Mpaka anaapishwa kuwa Rais wa Marekani inaelezwa simu aliyokuwa anatumia ni Samsung Galaxy S3 ambayo ilitolewa mwaka 2012.
Kwa upande wa Rais aliyepita Baraka Obama alisema wakati aningia madarakani alikuwa anatumia BlackBerry na matumizi yake yalikuwa ni kutuma ujumbe, kupiga picha na kusikiliza Muziki.

0 comments:

Post a Comment