Noti za dola 100
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwanamke mmoja nchini Colombia alitafuna na kumeza pesa zote
alizokuwa amejiwekea kama akiba, kuzuia mumewe asizichukue na kuzitumia.
Sandra Milena Almeida alimeza £7,000 ($9,000) baada ya
kugundua kwamba mumewe alikuwa na mpenzi mwingine.
Hatua yake iligunduliwa baada yake kukimbizwa hospitalini
akilalamika kutokana na maumivu makali tumboni.
Madaktari walipata mabunda ya noti katika tumbo lake.
Bi Almeida, 30, yamkini awali alificha pesa hizo baada ya
kusikia taarifa kwamba mumewe hakuwa mwaminifu kwake.
Lakini aliamua kuzila noti hizo za $100 baada ya mumewe
kugundua eneo alimokuwa ameficha pesa hizo na kudai agawiwe nusu yake.
Jamaa na madaktari waligundua kitendo alichokuwa amefanya
mwanamke huyo baada ya kumpima.
Noti zilizotolewa tumboni mwa Sandra.
Haki miliki ya
pichaREUTERS
Mkurugenzi wa
upasuaji katika hospitali ya chuo kikuu cha Santander, Juan Paulo Serrano,
aliambia wanahabari: "Noti 57 za $100 zilipatikana na kutolewa tumboni
mwake.
"Nyingine zilipatikana katika utumbo wake mkubwa."
"Yamkini kilikuwa kitendo cha kutamauka, kutokana na
tatizo lililomkabili. Hili bila shaka lilimwathiri tumbo."
Mrs Almeida, anayetoka Piedecuesta, anatarajiwa kupata nafuu
kabisa baada ya upasuaji huo.
Bw Serranoa anasema mwanzoni alidhani mwanamke huyo alikuwa
mlanguzi wa mihadarati Bw Serranoa anasema mwanzoni alidhani mwanamke huyo
alikuwa mlanguzi wa mihadarati
Bw Serrano alisema baadhi ya noti zilioshwa na zinaweza
kutumika tena.
Hata hivyo kunazo ambazo ziliathiriwa na kemikali tumboni.
Bi Almeida amesema sasa ataweka akiba pesa za kwenda likizo
ya kifahari.
SOURCE: BBC
0 comments:
Post a Comment