Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi London
Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.
Watu kumi na mmoja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London.
Kundi la Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo.
Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio la London ametajwa katika vyombo vya habari.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasio kuwa na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake.
Watu 21 waliojeruhiwa katika shambulio hilo wako katika hali mahututi.
0 comments:
Post a Comment