Friday, 2 June 2017
Home »
» Lowassa amponza Yericko Nyerere
Lowassa amponza Yericko Nyerere
Mfuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendele (Chadema) Yericko Nyerere amepandishwa Kizimbani na kusomewa mashtaka Matano yanayohusu kusambaza Taarifa za Uoungo kupita mtrandoa wa Facebook.
Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashuari wakili wa Serikali Athaas Elia amemsomea Nyerere mashtaka hayo pamoja na Kuandika kwenye ukuirasa wake wa Facebook Taarifa za kupotosha.
Wakili Elia alidai kuwa Nyerere siku ya Tarehe 25 Oktoba Mwaka 2015, sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam aliandika maneno haya" Mateso ya Ulimboka na Kibanda, Mateso ya kijana wetu wa JKT. Ukikumbuka haya fanya uamuzi sahihi bila ushabiki."
Shtka la Pili ni kuchapisha Taarifa ya uongo ambapo Tarehe 24 Oktoba Mwaka 2015 sehemu isiyojilikana Dar es Salaam, Nyerere aliindika kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa "Taifa la Tanzania kuanzia leo halihitaji AMANI, linahitaji Haki tu"
Shitaka la Tatu ni kuchapisha taarifa za uongo ambapo mshitakiwa katika ukurasa wake wa Facebook siku ya Tarehr 24 Oktoba mwaka 2015 aliandika kuwa "Siku ya leo mpaka siku ya kuapishwa Lowassa Taifa hili halihitaji AMANI bali Taifa hili linahitaji HAKI tu. Amani ilishatoweka siku nyingi, kilichosalia ni uvumilivu tu. Njia sahihi ya kulitibu Taifa hili ni kwa dola dharimu kutenda HAKI hata kama itawauma. Uchaguzi huu ni vita, anaedhani ni demokrasia apimwe akili. Hii ni vita kati ya UMMA na DOLA, ni vita kati ya wema na ubaya, ni vita kati ya shibe na njaa, ni vita kati ya masikini na matajiri"
Shitaka la la nne lilomkabili Nyerere ni kuchapisha taarifa za uongo ambapo tarehe 24 Agosti mwaka 2015 sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, kyupitia mtandao wa Facebook aliandika kuwa "Mipango ya hujuma ya JK toka Ngordoto Arusha muda huu. Kikwete yuko Ngordoto arusha na wakuu wote wa mikoa na Wilaya Tanzania nzima, Pia wakuu wa vyombo vya dola na wanadimu mbalimbali Wakuu wa Mikoa wanaelezwa kwamba kuwa NEC kwa kushirikiana na CCM tayari wameshatengeneza kura bandia kwa kutumia mfumo wa kalamu za kichina, pia wanaamuliwa kuhakikisha wanahujumu kampeni za UKAWA kwa kutumia vyombo vya dola"
Pia wanaagizwa kuhakikisha kamatakamata ya vijana bodaboda wiki moja kabla ya uchaguzi, na zaidi ni wakuu hao wa mikoa wanaagizwa wakawaagize ma DC kote nchini kuhakikisha wanalinda maslahi ya CCM popote walipo siku ya uchaguzi.
Shitaka la Mwisho ni la kuchapisha Taarifa za uongo pia ambapo mtuhumiwa aliiandika kwenye mitandao ya kijamii siku ya Terehe 3 Septemba mwaka 2015 aliandika kuwa HSBC BANK, NORTH LONDON BRANCH. Ccm has deposited 1.5 Pound Million fraudulently in favour of Dr Wilbroad Slaa Through his fuience Josephine Mushumbusi being Curruption from ccm to win Tanzania General Election 2015.
mshtakiwa amekana mashtaka yote na kudhaminiwa kwa shilingi 10 Milioni.
kesi hiyo itatajwa tena tarehe 5 mwezi juni mwaka huu.
SOURCE:MUUNGWANA
Related Posts:
Watu 8 wafariki baada ya kimbunga kugonga Afrika KusiniHaki miliki ya pichaIMAGE COPYRIGHTImage captionAlex De Kock alipiga picha hii akitazama kimbunga hicho kutoka kilima cha Signal Hill mjini Cape Town Watu 8 wamefariki baada ya kimbunga kikali kugonga mji wa Cape Town, Afrika… Read More
Kuna hofu abiria wote 120 waliokuwa kwenye ndege ya Burma, wamefarikiHaki miliki ya pichaAFPImage captionNdege ya Mizigo iliyopotea ikiwa na watu 120 Matumaini yanazidi kufifia kwa abiria wote 120, ambao walikuwa ndani ya ndege moja ya jeshi la Burma, iliyopotea angani ilipokuwa ikipaa katika … Read More
Watu 12 wauwawa katika shambulio la kwanza la 'IS' nchini IranHaki miliki ya pichaJAMARANNEWS/FARSImage captionPicha hii ya kituo cha Far News inaonyeha mlipuko nje ya kaburi Mashambulio mawili ya kujitoa mhanga katika Bunge la Iran na kwenye eneo la kaburi la kiongozi wa kidini Ayatoll… Read More
Wanaume wenye vipara katika hatari ya kuuliwa MusumbijiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionBaadhi ya watu wana imani potovu kuwa watu walio na upara wako na dhahabu kwenye vichwa vyao. Polisi nchini Musumbiji wameonya kuwa wamaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye ma… Read More
Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika NigeriaHaki miliki ya pichaOUPA MOKOENA/PRETORIA NEWSImage captionBw. Mnguni anaonekana akitafuna nywele za mwanadada huyu katika mojawepo ya mahubiri yake Afrika Kusini mwaka 2015 Kasisi mmoja anayejiita nabii na ambaye alisababish… Read More
0 comments:
Post a Comment