Dar es Salaam. Mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) sasa unasafirisha watu 200,000 kwa siku kutoka watu 50,000 iliyokuwa ikisafirisha mwaka jana baada ya mradi huo kuanza kazi.
Kuongezeka kwa idadi hiyo inaelezwa kuwa ni ishara ya wananchi kuukubali mradi huo na kuutumia kila siku waendapo sehemu zao za kazi au majumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliotembelea mradi wa BRT, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka Dar es Salaam (DART), Hazina Mfinanga amesema mafanikio ya mradi huo yametokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya wadau mbalimbali.
Mfinanga amewataja wadau hao kuwa ni kampuni ya UdaRT ambayo ndiyo inaendesha mabasi, Maxcom Africa ambao wanaendesha mifumo ya kukusanya nauli na benki ya NMB ambayo inasimamia upatikanaji wa fedha za mradi huo.
"Bado tuko kwenye kipindi cha majaribio wakati tukiendelea na mchakato wa kupanua njia za BRT katika jiji hili ili watu wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huu," amesema Mfinanga.
Mfinanga ambaye pia ni Meneja Rasilimali watu wa DART, amesema wazo la kuanzisha mradi huo lilikuwa ni kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Dar es Salaam ambazo ni pamoja na kupoteza muda kwenye foleni na uchafuzi wa mazingira.
SOURCE:MUUNGWANA
Friday, 2 June 2017
Home »
» Hii ndio idadi ya watu wanaosafiri kwenye mabasi ya mwendokasi kwa siku
Hii ndio idadi ya watu wanaosafiri kwenye mabasi ya mwendokasi kwa siku
Related Posts:
Man United kumtema Ibrahimovic Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionZlatan Ibrahimovic Timu ya Man united huenda isimuongeze mkataba mpya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 30. Zlatan mwenye miaka 35 ali… Read More
Uchaguzi Uingereza 2017: Mbwa wafika kwa wingi vituoniHaki miliki ya pichaTWITTER@KCATCLARKEImage captionFionn, Luna na Roby wakiwa kituoni wamiliki wao walipoenda kupiga kura Cumbria Wapiga kura walipokuwa wanafika vituoni kupiga kura Uingereza, mbwa wa kila aina hawakuachwa ny… Read More
England uso kwa uso na Venezuela fainali ya kombe la dunia U20Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMfungaji wa mabao mawili ya England Dominic Solanke katikati akishangailia na wachezaji wenzake Timu za England na Venezuela zimetinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe … Read More
Aliyeuwa na kujificha miaka 45 akamatwa Japan Haki miliki ya pichaAFPImage captionIdara ya polisi inasema kuwa imethibitisha kuwa kwa hakika ni mtoro Bw. Osaka, baada ya kuchunguza chembechembe za damu yake-DNA Kisa cha mshukiwa mmoja wa mauwaji nchini Japan, kim… Read More
Nini kitafanyika sasa baada ya uchaguzi Uingereza?Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES Nini kitafanyika kukikosekana mshindi wa moja kwa moja katika uchaguzi mkuu? Chama chenye wabunge wengi kitaunda serikali? Si lazima. Chama chenye wabunge wengi baada ya kura zote kuhesabiwa… Read More
0 comments:
Post a Comment